Mkopo wa Maendeleo

Wewe una ndoto, sisi tuna njia. Pata fedha za kufikia malengo yako ya ujenzi, biashara na malengo mengine.

Kuhusu Mkopo huu

Mkopo huu unatolewa kulingana na uwiano wa Akiba za mwanachama kwa madhumuni ya kufanikisha shughuli za kimaendeleo.

Huu ni mkopo unaoelekezwa katika shughuli za uzalishaji na ujenzi. Unatoa fursa kwa wanachama kupata mtaji wa kutosha kwa ajili ya kujenga nyumba, kununua eneo la majengo, kuanza au kupanua biashara, na kununua mali isiyohamishika.

Tunaamini kwamba maendeleo ya kifedha ya mwanachama ndiyo msingi wa maendeleo ya chama. Kwa hiyo, tunatoa masharti nafuu na riba nafuu ili kufanikisha malengo ya mwanachama.

Mkopo wa maendeleo unaweza kutumika kama ifuatavyo:

  • Ujenzi wa nyumba au maboresho ya makazi.
  • Kuanzisha au kupanua biashara.
  • Kilimo au uwekezaji katika sekta nyingine za uzalishaji.
  • Malipo ya elimu au shughuli nyingine za kuongeza maarifa.

Sifa za Mkopo wa Maendeleo

  • Mwanachama ataruhusiwa kukopa kiasi mara tatu (3) ya Akiba alizo nazo chamani.
  • Kiasi cha juu cha mkopo kitakuwa TZS 100,000,000/= (Milioni Mia Moja).
  • Muda wa juu wa marejesho wa mkopo huu ni miezi 60 (miaka 5).
  • Riba ya mkopo huu ni asilimia 15% Reducing Loan balance.
  • Mkopo huu unahamasisha ukuaji wa kiuchumi na ustawi wa wanachama wa ushirika.

Vigezo vya mkopo wa Maendeleo

  • Awe mwajiriwa wa Tazama Pipeline Ltd au fungamano lingine linalokubaliwa na chama
  • Awe mwanachama hai wa Tazama Saccos Ltd
  • Awe ametimiza Hisa kikanuni
  • Awe na akiba zinazohitajika

Uko Tayari Kuomba?

Wasiliana na ofisi zetu kupata ushauri zaidi kuhusu suala la dhamana na kuanza safari yako ya maendeleo.

Wasiliana Nasi