Mkopo wa Nipige Tafu ni mkopo ulioundwa mahsusi ili kuwasaidia wanachama kukabiliana na changamoto za kifedha za muda mfupi. Mkopo huu ni suluhisho rahisi na haraka kwa wanachama wanaohitaji msaada wa kifedha kwa matumizi ya dharura au mahitaji ya kibinafsi kama vile, Luku ya Umeme, Bill ya Maji, Ving’amuzi vya TV NK.
Matumizi yake ni kama:
Sifa za Mkopo wa Nipige Tafu:
Mkopo huu ni mkombozi wa haraka kwa wanachama, ukiwa na lengo la kuhakikisha kwamba matatizo ya kifedha hayawaathiri vibaya wanufaika.
Mkopo huu hutolewa bila kuzingatia Akiba za mkopaji
Kiasi cha juu cha mkopo huu, inategemea na uwezo wa kurejesha wa mwanachama
Muda wa juu wa marejesho wa mkopo huu ni Mwezi mmoja
Riba ya mkopo huu ni asilimia tano, kwa mwezi.
Tembelea ofisi zetu au tuandikie barua pepe wakati wowote unapotaka. Ikiwa una maswali yoyote, usisite kuwasiliana nasi.