Mkopo huu utatolewa kwa Mwanachama Mpya ambaye pia ni mwaajiriwa mpya wa TAZAMA PIPELINE LTD na watendaji wa TAZAMA SACCOS LTD kwa lengo la kumkarimu ili aweze kufanya mahitaji yake ya msingi ya Maisha wakati ndiyo anaanza kazi na TAZAMA PIPELINES LTD.
Mkopo huu unajikita katika dhana ya kusaidiana, kuhakikisha kuwa wanufaika wanapata msaada wa kifedha bila mzigo mkubwa wa marejesho, na matumizi yake ni kama:
Sifa za Mkopo wa Ukarimu:
Mkopo wa ukarimu ni njia ya kuonyesha mshikamano wa kweli, kusaidia wanachama kuondokana na changamoto za kifedha kwa njia ya huruma na upendo.
Mkopo huu hutolewa bila kuzingatia Akiba za mkopaji.
Kiasi cha juu cha mkopo huu, inategemea na uwezo wa kurejesha wa mwanachama.
Muda wa juu wa marejesho wa mkopo huu ni Miezi 24, au miaka 2.
Riba ya mkopo huu ni asilimia kumi na tano, Reducing Loan balance.
Tembelea ofisi zetu au tuandikie barua pepe wakati wowote unapotaka. Ikiwa una maswali yoyote, usisite kuwasiliana nasi.