Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo TAZAMA (TAZAMA SACCOS Ltd) kilianzishwa rasmi Tarehe 14/04/ 1976 na kusajiriwa chini ya sheria ya Ushirika ya Mwaka 1968 na kupewa hati ya Na. DSR. 88. Na sasa Hati Na PRI-DAR-KGM-MC-2022-464.
Ukiwa Ushirika wenye dhima ya kikomo (DYK), Wanachama wake walitokana na Utumishi ulio chini ya Kampuni ya usafirishaji mafuta (TANZANIA ZAMBIA MAFUTA).
Kijiografia ushirika huu unafanya kazi kanda ya Tanzania Bara kwa kuwa na wanachama kwenye vituo vyote vya TAZAMA PIPELINES Ltd ambavyo ni Dar es Salaam, Morogoro,
Elphones’ Pass, Iringa na Mbeya; na Dar es Salaam ndiyo makao makuu ya chama.
Lengo kuu la kuanzishwa kwake lililenga kuunganisha nguvu za kiuchumi za baadhi ya waajiriwa mmoja mmoja, wanachama kuunda Mtaji wa pamoja kwa njia ya kujiwekea Akiba mara kwa mara ili kujipatia huduma za kifedha na zisizo za kifedha kuwawezesha kuondoa kero zao zitokanazo na umasikini wa kipato.
Mwaka 1976 Ushirika ulianza na wanachama 25, na ilipofika 1983 walikuwa 50 na baadaye kuongezeka kila mwaka na kufikia mwaka 2024 wanachama hai wapo 271.
Ushirika huu ulianza ukiwa na wanachama 25.
Idadi ya Wanachama Hai tulionao mpaka 2024.
Ushirika unaendeshwa na wafanyakazi wa kudumu.
Timu yetu ni madhubuti kutoa na kukusanya mikopo.
Kukidhi na kuzidi matarajio ya wanachama na kuwa mojawapo ya SACCOS zilizofanikiwa na zinazoendeshwa vyema nchini Tanzania.
Kuhamasisha akiba, kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanachama wetu kwa ajili ya maendeleo, na kuhakikisha marejesho ya hiari kupitia bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wanachama wetu.
Kiongozi mkuu wa ushirika, TAZAMA.
Utendaji wa chama kila siku.
Utendaji wa chama kila siku.
Kiongozi mkuu wa ushirika, TAZAMA.
Utendaji wa chama kila siku.